AFISA URASIMISHAJI WA BIASHARA- NAFASI 1 - 1 POST

Employer: Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge - Mkurabita
Date Published: 2019-02-07
Application Deadline: 2019-02-21

JOB SUMMARY:

Kushiriki katika kujenga uwezo wa Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, anawajibika katika utekelezaji wa shughuli za urasimishaji na uendelezaji wa biashara ambazo zinatekelezwa kwa kutumia Mfumo wa Kituo Kimoja Cha Urasimishaji na Uendendelezaji wa Biashara katika Mamlaka za Mitaa za Tanzania.

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

i.Kuandaa na kutunza Kazi Data ya biashara  zinazopatikana katika Halmashauri, Miji na Majiji ambayo urasimishaji unafanyika ili kubaini hali ya biashara kabla na baada ya urasimishaji;

ii.Kushiriki katika kuhamasisha Halmashauri, Miji na Majiji ili yatenge maeneo/majengo kwa ajili ya kuanzisha na kuendesha Vituo vya Urasimishaji na uendelezaji wa biashara; 

iii.Kushiriki katika Kuandaa na Kuendesha mafunzo ya Urasimishaji na uendelezaji wa biashara katika Vituo vya Urasimisahaji na Uendelezaji wa Biashara vinavyoanzishwa katika Halmashauri, Miji na Majiji ya Tanzania;

iv. Kuandaa na kutekeleza Mpango Kazi na Bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa urasimishaji na uendelezaji wa biashara katika Halmashauri, Miji na Majiji ya Tanzania;

v.Kupokea na kuchambua taarifa za utekelezaji wa shughuli za urasimishaji na uendelezaji wa biashara katika Vituo vya Uarasimishaji ambavyo vitakuwa viananzishwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Tanzania; 

vi.Kushiriki katika Kampeni ya kuhamasisha Vijana kubuni, kuanzisha na kuendesha Biashara na Viwanda Vidogo kwa kutumia fursa ambazo zipo katika mazingira yao.

vii.Kushirikiana na Afisa Utafiti, Ufuatiliaji na Tathmini kufanya ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa urasimishaji na uendelezaji ambao unafanyika kwa kutumia Vituo vya Urasimishaji na Uendelezaji wa biashara katika Halmashauri, Miji na Majiji ya Tanzania.

 


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

Awe na Shahada ya Utawala wa Biashara (Business Administration), Entrepreneurship au zingine zenye uhusiano na  kazi hii ambazo zinatambulika na Mamlaka ya Usimamizi wa Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania; Awe na uzoefu wa miaka mitatu (3) kuhusu Sheria, Kanuni na Taratibu za Usajili, Usimamizi na Uendelezaji wa biashara za Tanzania;

 

REMUNERATION: Salary Scale Attractive remuneration

Login to Apply