AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURAL OFFICER II) - 3 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2019-08-06
Application Deadline: 2019-08-20

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

i.Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,

ii.Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi.,

iii.Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/mwezi,

iv.Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,

v.Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,

vi.Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,

vii.Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,

viii.Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,

ix.Kuaandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo  ya mazao, 

x.Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine,

xi.Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,

xii.Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,

xiii.Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,

xiv.Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,

xv.Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,

xvi.Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,

xvii.Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,

xviii.Kufanya utafiti wa udongo

xix.Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulim/wamwagiliaji,

xx. Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti; na

xxi.Kuendesha/kusimamia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

Kuajiriwa wenye shahada ya Kilimo au shahada ya Sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

 

REMUNERATION: Salary Scale TGS.D

Login to Apply