AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER II)., - 12 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2019-08-06
Application Deadline: 2019-08-20

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

i.Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake;

ii.Kwa kushirikiana na wakaguzi wa afya, atakagua nyama na usafi wa machinjio mara kwa mara;

iii.Atakusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo kama ngozi na kuandika ripoti;

iv.Atatibu magonjwa ya mifugo chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo na kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa;

v.Atatembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam katika eneo lake la kazi;

vi.Atakusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake;

vii.Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundo mbinu inayohusiana na ufugaji bora;

viii.Atahusika na uhamilishaji (Artificail Insemination) na uzalishaji (breeding) wa mifugo kwa ujumla;

ix.Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa ndama;

x.Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi wa kazi.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliofuzu mafunzo ya Stashahada (DIPLOMA) ya mifugo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo (MATI au LITI) au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.

 

REMUNERATION: Salary Scale TGS C;

Login to Apply