MENEJA WA URASIMISHAJI RASILIMALI MIJINI - 1 POST

Employer: Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge - Mkurabita
Date Published: 2019-10-02
Application Deadline: 2019-10-16

JOB SUMMARY:

Kujenga uwezo wa urasimishaji wa ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Ambazo zinatekeleza urasimishaji wa ardhi Tanzania. Aidha, anawajibika kusimamia na kuratibu shughuli za urasimishaji wa ardhi ambazo zinatekelezwa Tanzania Bara.

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

i.    Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za urasimishaji ardhi Mijini Tanzania Bara;

ii.    Kuandaa na kufanya Mapitio ya Miongozo ya mafunzo kwa ajili ya kujenga uwezo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara;

iii.    Kuandaa na Kuendesha mafunzo ya Urasimishaji wa ardhi Mijini kwa Wataalam wa sekta ya ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Tanzania Bara;

iv.    Kuandaa na kutekeleza Mpango Kazi na Bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa urasimishaji wa ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara;

v.    Kupokea na kuchambua taarifa za utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa ardhi Mjini ambazo zinatekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

za Tanzania Bara;

vi.    Kubainisha na kutoa ushauri wa utatuzi wa changamoto ambazo zinabainika wakati wa utekelezaji wa urasimishaji wa ardhi Mjini Tanzania Bara;

vii.    Kufanya tathimini na kupendekeza maboresho ya Kisheria, Kanuni na Kitaasisi ambazo zinabainika kuendelea kuwa kikwazo kwa Wananchi katika kurasimisha ardhi zao Mijini na Majiji ya Tanzania Bara;

viii.    Kuandaa na kutunza Kazi Data ya Rasilimali ardhi  zilizorasimishwa katika

Miji na Majiji ya Tanzania Bara;

ix.    Kushirikiana na Mtaalamu wa Mawasiliano kwa Umma katika kuhamisisha na kujenga hamasa kwa wamiliki wa ardhi mijini ili waweze kurasimisha rasilimali zao;

x.    Kuandaa na kufanya mapitio vigezo inavyotumika kuchagua ya kufanya urasimishaji kila mwaka katika Miji na Majiji ya Tanzania Bara; na

xi.    Kazi zingine ambazo utapangiwa na Msimamizi wako wa kazi.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

i.    Awe na Shahada ya Upimaji na Ramani au Usimamizi na Utawala wa Masuala ya Ardhi ambayo inatambulika na Mamlaka ya Usimamizi wa Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania;
ii.    Awe na uzoefu wa miaka mitano (5) kuhusu Sheria, Kanuni na Taratibu za Upimaji, Usimamizi na Usajili wa Ardhi za Tanzania Bara; na
iii.     Awe na uzoefu katika utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa Ardhi Mijini na Majiji ya Tanzania Bara.

REMUNERATION: Salary Scale Attractive remuneration

CLOSED 7 day(s) Ago.