MSAJILI MSAIDIZI WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WA WILAYA - 1 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

KAZI/MAJUKUMU YA MSAJILI MSAIDIZI WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA

Msajili Msaidizi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Wilaya atakuwa na Majukumu yafuatayo:
i.    Kusimamia utekelezaji wa sheria  Na. 2 ya mwaka 2002;
ii.    Kuelimisha Umma kuhusu mfumo mpya wa utatuzi wa migogoro ya Ardhi na Nyumba;
iii.    Kushirikiana wa Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya kuhakikisha kuwa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji yanaundwa na Mabaraza ya Kata yanafufuliwa na yote yanafanya kazi kwa mujibu wa sheria husika;
iv.    Kuhakikisha kuwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yanakuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi; Pale ambapo hakuna ofisi, kuwasiliana na viongozi wa Mkoa/Wilaya kuhakikisha kuwa ofisi zinapatikana/Majengo yanapatikana.
v.    Kuhakikisha kuwa kila Baraza lina wajumbe kulingana na matakwa ya Sheria na kama kuna upungufu kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa ili atume mapendekezo kwa Mheshimiwa Waziri;
vi.    Kuhakikisha kuwa Mabaraza yana vitendea kazi vya kutosha;
vii.    Kuratibu vikao vya Mabaraza kwa ushirikiano na Wenyeviti;
viii.    Kuhakikisha kuwa Taarifa ya utekelezaji (Return) ya kila mwezi inaandaliwa kwa usahihi na kutumwa kwa Msajili;
ix.    Kusimamia utayarishaji wa nyaraka mbalimbali zinazohusiana na marejeo, rufaa, nk na kuhakikisha kuwa zinapelekwa Mahakama Kuu- Kitengo cha Ardhi kwa wakati;
x.    Kusimamia utendaji kazi wa Madalali wa Baraza;
xi.    Kuhakikisha kuwa fedha zinazokusanywa katika Mabaraza kutokana na ada mbalimbali katika Mabaraza zinapelekwa Benki kwa wakati na kuwa fedha za matumizi zinatumwa katika Mabaraza kama ilivyokusudiwa;
xii.    Kuhakikisha kuwa taarifa za makusanyo na matumizi (uthibitisho wa jinsi fedha zilivyotumika) zitumwe kwa Katibu Mkuu kila mwezi.
xiii.    Kuhakikisha kuwa Watumishi wanapata haki zao;
xiv.    Kusikiliza malalamiko ya wananchi;
xv.    Kufanya kazi zingine kama utakavyoelekezwa na Mkuu wako wa kazi.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

SIFA ZA MWOMBAJI
Shahada ya Sheria  kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na awe amemaliza mafunzo ya kazini internship/Externship au mafunzo ya Shule ya Sheria (Law School), uzoefu wa miaka mitano (5) na kuendelea katika masuala ya Sheria, awe mwadilifu na asiye na historia ya makosa ya jinai na awe na umri usiopungua miaka thelathini na tano (35)

REMUNERATION: Salary Scale TGS I.

Login to Apply