MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) WATER RESOURCE ENGINEER. - 20 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

i.    Kufanya upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira;
ii.    Kufanya mapitio ya taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira;
iii.    Kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa;
iv.    Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira;
v.    Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;
vi.    Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji;
vii.    Kusimamia, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
viii.    Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

•    Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

REMUNERATION: Salary Scale TGS.E

Login to Apply