MSAIDIZI WA MTENDAJI MKUU DARAJA LA II (ASSISTANT EXECUTIVE SECRETARY) - 2 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

i.    Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida;
ii.    Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
iii.    Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi na wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa;
iv.    Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini;
v.    Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao;
vi.    Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika;
vii.    Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali mahali alipo;
viii.    Kutoa taarifa na kufuatiliapanapohusika kuhusu matengenezo yam ashine za kazi;
ix.    Kuandika muhtasari wa vikao vinavyohusika sehemu alipo na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya vikao hivyo;
x.    Kuandika barua zinazotoa taarifa ya ratiba ya shughuli au safari za mkuu wake na kuitisha vikao;
xi.    Kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya mkuu wake sehemu mbalimbali.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

•    Kuajiriwa wenye stashahada ya kawaida ya Uhazili itolewayo na chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali ambao wamehudhuria mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za'' Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher''. Pia wawe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka kumi na mbili. Aidha wawe wamehudhuria na kufaulu mtihani wa mafunzo ya menejimenti kwa ajili ya wasaidizi wa watendaji wakuu kutoka chuo cha utumishi wa Umma (TPSC) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na serikali.

REMUNERATION: Salary Scale TGS F

Login to Apply