AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI II (ASSISTANT COMMUNITY DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) - 18 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

NA

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

• Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya jamii katika Kijiji zikiwemo za wanawake na watoto na zikizingatia jinsia.
• Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia, kutathmini mipango/miradi ya maendeleo.
• Kuhamasisha na kuwawezesha wanachi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora vijijini, ujenzi wa shule, zahanati, majosho, barabara za vijijini (Feeder Roads), uchimbaji wa visima vifupi na uchimbaji wa marambo.
• Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo vya maendeleo hasa vya maji na nishati kwa kuwa na miradi ya uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu na matumizi ya mikokoteni.
• Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa viongozi wa kijiji na vikundi mbalimbali vya maendeleo kijijini kuhusu:-
- Utawala bora na Uongozi
- Ujasiriamali
- Mbinu shirikishi jamii na kazi za kujitegemea
- Chakula bora na lishe
- Utunzani na malezi bora ya watoto
• Kuwa kiungo kati ya wanakijiji (Afisa Mtendaji wa Kata) na watumishi wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo.
• Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea
• Kuwawezesha wananchi kubaini na kuratibu rasilimali zilizopo  na kuzitumia katika miradi ya kujitegemea
• Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kuwasaidia wananchi kutumia takwimu na kumbukumbu mbalimbali za kijiji.
• Kuwawezesha viongozi wa vijiji kutumia mbinu shirikishi jamii kuandaa ratiba za kazi na mipango ya utekelezaji.
• Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata.
• Kuhamasisha na kuwezesha jamii kuona umuhimu wa kuthamini mazingira kwa kutumia mazingira kwa njia endelevu na hasa kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vya baadae
• Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo
• Kuratibu shughuli za Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali na za kijamii
• Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

•Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV/VI wenye Stashahada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (Buhare au Rungemba) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

REMUNERATION: Salary Scale TGS.D

Login to Apply