MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE GRADE II). - 28 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:


i.    Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya Kata;
ii.    Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini;
iii.    Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya Kata;
iv.    Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya Kata, Vijiji na Mtaa;
v.    Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake;
vi.    Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Kata;
vii.    Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake;
viii.    Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya Kata;
ix.    Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa;
x.    Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake;
xi.    Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika Vijiji, Vitongoji, na Kata yake.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:


•    Kuajiriwa wenye Shahada yenye mwelekeo wa Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment) au Sheria kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

REMUNERATION: Salary Scale TGS.D

Login to Apply