AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II). - 3 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:


i.    Kuratibu mipango ya uzalishaji mifugo wilayani;
ii.    Kuratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo;
iii.    Kusaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani;
iv.    Kuratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji;
v.    Kufanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani;
vi.    Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani;
vii.    Kufanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi;
viii.    Kuendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo;
ix.    Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali ;
x.    Kufanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya;
xi.    Kushiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho;
xii.    Kuandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo;
xiii.    Kufuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo;
xiv.    Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:


•    Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Mifugo (Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana nayo.

REMUNERATION: Salary Scale TGS.D

Login to Apply