AFISA TARAFA. - 7 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu
i.    Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa;
ii.    Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya;
iii.    Kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa;
iv.    Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi kwenye Tarafa;
v.    Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake;
vi.    Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo;
vii.    Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake;
viii.    Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya;
ix.    Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa katika eneo lake;
x.    Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.

(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa
i.    Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake;
ii.    Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa;
iii.    Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake;
iv.    Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri;
v.    Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata;
vi.    Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:


•    Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Sheria, Menejimenti, Utawala, Kilimo, Mifugo, Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

REMUNERATION: Salary Scale TGS.D

Login to Apply