AFISA UTALII DARAJA LA II.. - 1 POST

Employer: MDAs & LGAs
Date Published: 2017-08-24
Application Deadline: 2017-09-08

JOB SUMMARY:

N/A

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

i.    Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na wadau wote;
ii.    Kutoa Leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii;
iii.    Kukusanya na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii;
iv.    Kutafuta na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi;
v.    Kujibu malalamiko kutoka kwa watalii;
vi.    Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wadau katika uendeshaji wa Biashara ya utalii.
vii.    Kuandaa kaguzi mbalimbali za Wakala wa utalii;
viii.    Kuchambua miradi ya wakala wa utalii na hoteli;
ix.    Kukagua hoteli, loji na migahawa;
x.    Kujibu na kufatilia malalamiko yanayoletwa na watalii;
xi.    Kutoa ushauri wa kiutaalam kwa wakala wa utalii;
xii.    Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na Washika dau wote;
xiii.    Kukusanya takwimu za watalii kwenye sehemu/vituo nchini vya kuingilia/kutoa wageni;
xiv.    Kutunza kumbukumbu za vitabu/majalada ya Maktaba ya Utalii;
xv.    Kutayarisha taarifa ya kila mwezi ya takwimu za watalii waliongia nchini na mapato yaliyopatikana;
xvi.    Kufanya tafiti ngo “Survey” kwenye Hifadhi za Taifa na maeneo tengefu ili kupata idadi kamili ya Hoteli au Loji zinazotoa huduma kwa watalii;
xvii.    Kufuatilia kwa karibu na kushirikiana na VETA juu ya maendeleo ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini;
xviii.    Kuratibu miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii;
xix.    Kutayarisha ripoti za mwezi, robo mwaka, na za mwaka mzima;
xx.    Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Sekta kwa kufanya ‘‘survey’’;
xxi.    Kuitisha mikutano ya Tourism Facilitation Committee;
xxii.    Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe na kukufuatilia utekelezaji wa maazimio;
xxiii.    Kupitia miongozo inayohusu “Tourism Facilitation Committee”;
xxiv.    Kuratibu shughuli za kubuni vivutio vya utalii na mienendo mipya ya kuendeleza utalii;
xxv.    Kutayarisha kuhakiki vivutio vya utalii nchini;
xxvi.    Kuitisha mikutano/semina za uhamasishaji kuhusu uendelezaji utalii;
xxvii.    Kushiriki katika kupitia ripoti za tathmini ya athari za kimazingira (EIA) kuhusu miradi ya utalii;
xxviii.    Kushirikiana na Mashirika/taasisi mbalimali za mazingira katika shughuli zihusuzo utalii na mazingira;
xxix.    Kukusanya rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje.


QUALIFICATION AND EXPERIENCE:

•    Kuajiriwa wenye Shahada/stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Utalii au Hoteli kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

REMUNERATION: Salary Scale TGS.D

Login to Apply